Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy azindua huduma ya dharura kwa wagonjwa mahututi

69574 Pic+ummy

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Idadi ya wagonjwa wanaokufa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo itapungua kwa asilimia 40 kufutia kuzinduliwa kwa huduma ya dharura na wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Huduma hiyo imezinduliwa leo Ijumaa Agosti 2, 2019 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya kukamilika kwa ukarabati wa majengo ya huduma hizo kwa Sh350 milioni.

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Leonard Subi amesema utafiti unaonyesha huduma ya dharura na ya wagonjwa mahututi itapunguza vifo kwa asilimia 40.

“Bombo imekuwa ya kwanza nchini kufunguliwa kwa huduma kati ya hospitali 28 za Mikoa nchini. Tutaendelea kufungua katika hospitali nyingine baada ya Bombo itafuatia ya Dodoma, Mwanza,”amesema Dk Subi.

Subi ambaye pia ni mkurugenzi wa huduma za kinga wa Wizara ya Afya amesema tangu kufunguliwa huduma kama hiyo katika hospitali ya ya Taifa Muhimbili (MNH), idadi ya vifo imepungua  kutoka asilimia 13 hadi saba.

Naibu Rais wa mfuko wa Abott uliotoa kiasi hicho cha fedha, Andrew Willson amesema mfuko huo

Pia Soma

utafadhili ukarabati na ujenzi wa majengo ya huduma kama hiyo katika hospitali nyingine mbili nchini Tanzania ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli anazofanya kuimarisha sekta ya afya.

“Abott inaunga mkono mapinduzi anayoyafanya Rais John Magufuli katika kuiletea maendeleo Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya,” amesema  Willson.

Akizungumza baada ya uzinduzi, Ummy amesema kupitia huduma hiyo, wagonjwa wanaofikishwa wataweza kupata huduma zote za vipimo pamoja na matibabu ndani ya vyumba vya dharura kabla ya kupumzishwa

wodini.

“Haya ni mapinduzi kwa sababu katika jengo la dharura kuna vitanda 12, hii ina maana wagonjwa wengi wataweza kuhudumiwa kwa wakati mmoja,” amesema Ummy.

Chanzo: mwananchi.co.tz