Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy awataka wadau kuwekeza kwenye ajira za afya

LISHE NA UMMY Ummy Mwalimu, Waziri TAMISEMI

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amewataka wadau wanaotekeleza Afua za nchini kuwekeza kwenye ajira za watumishi wa Afya ili kukabiliana na upungufu wa watumishi wa kada hiyo uliopo hivi sasa.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa kufunga mradi wa USAID Boresha Afya Kanda ya Kaskazini, Kati na Kusuni iliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Amesema changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wadau ambao wametekeleza kazi za mradi huo ni pamoja na upungufu wa watumishi, changamoto ambayo Serikali inaitambua na inatoa kipaumbele na kuwa tayari wameshapeleka maombi ya kibali cha ajira utumishi kwaajili ya kuajiri wataalamu hao

“Watumishi wa Afya waliopo hivi sasa ni 47% tu ya mahitaji hivyo tuna upungufu wa 53% hata tukiajiri hatuwezi kumaliza tatizo hili hivyo ni vyema na wadau wetu mkatuunga mkono” amesema Ummy.

Ameongeza kusema kuwa kila Mdau akiweka kipengele cha kuajiri wataalam wa Afya hata wawili tu kwa mwaka itasaidia katika kuboresha eneo hilo kwa pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live