Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy atoa somo kwa chama kipya cha Urembo na Vipodozi Tanzania

73027 Pic+ummy

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar ea Salaam. Licha ya sekta ya Urembo na Vipodozi inakua kwa haraka duniani  kwa kiasi cha Sh50 trilioni katika soko la dunia  kwa mwaka, Tanzania imetajwa kutofanya vizuri kwani inapata asilimia tatu pekee ya kiasi hicho cha fedha.

Kwa mantiki hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kuwa sekta hiyo inayozalisha ajira kwa vijana inapewa hadhi ili iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Ummy ameyasema hayo leo Jumatatu Agosti 26,2019 wakati wa uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) yenye kauli mbiu isemayo ‘Urembo na vipodozi kwa afya na uchumi wa viwanda’.

Lengo la kuunda chama hicho ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara, wauzaji na watengenezaji wa vipodozi kuwa na sauti moja ili kufanikisha sekta hiyo iweze kusonga mbela.

“Niwapongeze kwa kuunda chama hichi ambacho kitawatambulisha popote duniani,  lakini pia kwa kuwa pamoja mtaweza kubaini wale wote ambao ana uhakika katika kutengeneza vipodozi vyenye viambata sumu,” amesema Waziri Ummy.

Aidha amewataka wanachama hao kuzingatia sheria na afya kwa kuzalisha bidhaa ambazo hazina madhara kwa mtumiaji ili kuepuka madhara yatokanayo na vipodozi bandia.

Pia Soma

“Na nitoe tu rai kwa wananchi kuwa na ushirikiano mkibaini mtu yeyote anayeuza ama kutengeneza vipodozi vyenye viambata sumu mnatoa taarifa ili tuweze kuchukua hatua za kisheria,”ameongeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser amesema ili kukuza sekta hiyo Tanzania inapaswa kuwa na mikakati ili iweze kukua kama ilivyo nchi za Afrika ya Kusini na Nigeria.

Chanzo: mwananchi.co.tz