Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy ataka viongozi wa dini kuhamasisha chanjo

Waziri Ummy Mwalimu . Waziri Ummy Mwalimu

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: Mwananchi

Serikali imewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanahamasisha na kuelemisha waumini wao ili wajitokeze kuchanja chanjo ya uviko 19.

Wito huo umetolewa jana Julai 20 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha mashauriano na majadiliano ya viongozi wa dini mkaoni humo kuhusu maambukizi ya Uviko 19.

"Haijulikani kirusi kitakachokuja kitakuwa na ukali kiasi gani hivyo himizeni waumini wenu wakachanje ili wawe salama," amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa imethibitika kuwa chanjo ndio njia pekee yakuweza kupunguza makali ya ugonjwa wa corona na ndio maana Rais Samia Suluhu alizindua kampeni ya uchanjaji na yeye na viongozi wengine walichanja.

Ummy amesema kuwa  hadi kufikia Julay 18 wamechanjwa watu milion 11.5 ambao wamechanjwa dozi kamili, huku lengo la Serikali likiwa ni kuchanja watu milion 30.7.

Amesema ili kutengeneza kinga ya jamii, dunia imejiwekea malengo ya kuchanja angalau asilimia 70 ya watu wote duniani na kwamba Tanzania imekadiriwa tuna watu milion 59 hivyo wachanje watu asilimia 70.   

Advertisement "Mimi nikaona tunajidanganya nikaona ni badili malengo na ninashukuru Rais ameridhia, hivyo tumesema tutachanja watu asilimia 70 Kwa kuchanja watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea," ameeleza Ummy.

Amesema mpaka sasa kiwango kilichofikiwa ni asilimia 37 ya watu wenye umri wa miaka 18 kuendelea na Tanga ina asilimia 22, ambacho ni chini ya kiwango cha kitaifa.

"Viongozi wa dini tumieni siku za ibada kuhamasisha kucha kwani hatujui kirusi kitakachokuja kinakuja na ukali gani, chanjo ni salama na chanjo hizi zimethibitika pasina shaka kuwa ni njia ya haraka ya kupunguza makali ya uviko 19 hivyo kuto chanja unajiweka katika hatari zaidi," amesema Waziri huyo wa Afya.

Naye mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef), Mei Bukuku amewaomba viongozi wa dini kuwaruhusu watoa huduma kutoa chanjo kwa waumini kwenye nyumba za ibada.

Awali Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Dk Emalberga Kasangala amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya watu kurudi kuchanjwa dozi ya pili ya chanjo ya uviko 19.

Hata hivyo, amesema Serikali imekuwa ikitekeleza mikakati ya kudhibiti maambukizi Kwa kuhamasisha na kutoa elimu Kwa jamii, utekelezaji wa huduma mkoba na tembezi .

Chanzo: Mwananchi