Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy asikia kilio ajira wataalamu wa maabara

Waziri Ummy Asikia Kilio Ajira Wataalamu Wa Maabara Waziri Ummy asikia kilio ajira wataalamu wa maabara

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amemwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya kufanya uchambuzi wa kina kwenye kada za Afya kuanzia ngazi ya Taifa mpaka Zahanati ikiwemo kada ya Wataalamu wa Maabara ili kuweka kipaumbele sahihi katika kuajiri Wataalamu wa kada ambazo zina upungufu mkubwa katika Sekta ya Afya kulingana na mahitaji ya nchi.

Waziri Ummy amesema hayo akiwa anajibu hoja za wataalam wa maabara waliohoji mitandaoni kuhusu changamoto ya ajira za wataalam wa maabara zinazotolewa na Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Wataalam wa Maabara ni kada muhimu katika utoaji huduma bora za Afya, ni kweli kuwa tiba sahihi ya ugonjwa inategemea huduma za uchunguzi wa magonjwa (Maabara na Radiolojia). Kuhusu idadi ndogo ya Wataalam wa Maabara nimesikia kilio chenu na tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu,” amesema Waziri Ummy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live