Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amekutana na wataalam wa afya na kujadili hali ya mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha wizara hiyo leo Ijumaa Machi 20, 2020 imesema kuwa katika kikao hicho cha Waziri Ummy na wataalamu hao wa afya wamejadili mambo manne.
Jambo la kwanza lililojadiliwa kwenye kikao hicho ni kuhakikisha hospitali za Serikali na binafsi zinazingatia miongozo ya Wizara kuhusu magonjwa ya mlipuko kabla ya kuwahamisha wagonjwa kwenye hospitali za rufaa za Serikali.
Jambo la pili lililojadiliwa kwenye kikao hicho ni kuitaka Serikali kuendelea kutoa elimu na maelezo sahihi kwa wananchi kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona, dalili zakje na hali halisi ya mweenendo wa ugonjwa huo nchini.
Suala lingine ambalo kikao hicho kimejadili ni kuvishauri vyombao vya habari kutumia waataalam wa afya kutoka wezara ya afya na taasisi zake pamoja na waganga wakuu wa mikioa na halmashauri ili kuhakikisha mnaudhui ya uelimishaji kuhusu ugonjwa huo ni sahihi.
Katika kikao hicho cha waziri Ummy na wataalamu wa afya pia wamewataka wananchi kupuuza taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii zinazotolewa na baadhi ya watu zinazopotosha hali halisi ya ugonjwa wa corona nchini.
Habari zinazohusiana na hii
- Jinsi dereva wa basi la Isamilo alivyofariki akiwa safarini
- Agizo la Latra kuhusu kujikinga na corona lapata ugumu kutekelezwa
- Corona ilivyobadili taratibu makanisani
- FCC yaonya upandishaji bei vifaa vya kujikinga corona Tanzania
“Hadi kufikia Machi 20, 2020 Tanzania imethibitisha kuwepo kwa kesi 6 za wagonjwa wa corona ambao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa watumishi wa sekta ya afya” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Wizara ya Afya inaendeleaa kutoa huduma ya afya kwa watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona na kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa huo.