Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy abainisha mambo matatu ya kutofautisha hospitali na vituo vya afya

65084 Pic+ummy

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ametaja maeneo matatu muhimu katika mpango wa muda mfupi na mrefu katika hospitali za rufaa za mkoa ili kuzitofautisha na vituo vya afya.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jumatatu Julai 1, 2019 jijini Dodoma, Tanzania wakati akifungua mkutano wa viongozi wa hospitali za rufaa za mkoa.

Amesema maeneo hayo matuta yakipatiwa ufumbuzi yatasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo.

Ameyataka maeneo hayo ni kila hospitali ya rufaa za mikoa kuwa na madaktari bingwa katika huduma za kibingwa 13 akitole mfano huduma ya moyo, kinywa, masikio, meno pamoja na huduma ya mama na mtoto.

Pili, miundombinu hususani katika huduma za ICU, pamoja na  huduma za dharura na ajali.

Waziri Ummy ametaja jambo la tatu ni mama na mtoto hususani huduma ya ICU ya  mama pamoja na ya mtoto.

Pia Soma

Hata hivyo amewataka viongozi hao kupitia kikao chao kuangalia maeneo mengine ambayo yanaweza kutekelezwa katika mpango huo wa muda mfupi na mrefu.

Amesema kupitia utekelezaji huo hospitali hizo zitakuwa mfano kwa vituo vya afya vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa afya, Dk Faustine Ndungulile amesema bado wanapokea malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na baadhi ya watumishi wa taasisi.

Amesema kazi ya waganga wafawidhi sio kukaa ofisini bali ni kusikiliza na kutumia changamoto mbalimbali akisema ni lazima kuwa na mfumo mzuri wa kutatua malalamiko hayo.

Hata hivyo, alikumbushia agizo la kila mtumishi wa afya kuwa na kitambulisho ili kuwabaini wale wote wanaofanya kazi bila kuzingatia miiko ya kazi.

Alisema hiyo itasaidia kukaa nani kafanya nini na kwa wakati gani.

Kuhusu suala la mapato amesema hospitali za rufaa za mkoani zitashindanishwa katika ukusanyaji wa mapato akisema fedha hizo zinasaidia kuimarisha huduma za afya.

Chanzo: mwananchi.co.tz