Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy aagiza uchunguzi zaidi 'energy drink'

Waziri Ummy Mwalimu . Waziri Ummy aagiza uchunguzi zaidi 'energy drink'

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ametoa maelekezo kwa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti zaidi kuhusu suala la matumizi ya energy drink.

Kauli hiyo ya Ummy imekuja kufutia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kuripoti madhara ya matumizi ya energy drink kwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 28.

"Nimeielekeza Taasisi yetu ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu @NIMR_Tanzania kufanya utafiti zaidi kuhusu suala hili la matumizi ya Energy Drink na kutupa ushahidi wa kisayansi ili tuweze kuchukua hatua stahiki," aliandika Ummy kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kisa hicho kipya ambacho ni nadra kutokea kimechapishwa katika Jarida Maarufu la Kisayansi la Marekani la SAGE journal ambapo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliripoti madhara ya matumizi ya energy drink kwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 28.

Kijana huyo wa Kitanzania alipata tatizo la maumivu makali upande wa kulia wa kifua huku dawa za kutuliza maumivu kugonga mwamba na kupelekwa hospitali kwa haraka.

Katika maelezo yake kwa madaktari wa JKCI kijana huyo ameeleza namna alivyokunywa kinywaji wa kuongeza nguvu (energy drink) kopo tano mfululizo na baada ya muda mfupi kuanza kupata maumivu hayo.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo JKCI, Dk Pedro Pallangyo amesema Katika historia ya awali ya kijana huyo hakuwa na sababu hatarishi za magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyoambukiza kama sababu hatarishi tano za uvutaji sigara, unywaji pombe kupindukia, kutofanya mazoezi, uzito na ulaji usiofaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live