Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy aagiza muuguzi anayetuhumiwa kubaka mjamzito asimamishwe kazi

89380 Ummy+pic Waziri Ummy aagiza muuguzi anayetuhumiwa kubaka mjamzito asimamishwe kazi

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu  ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani Katavi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 20, 2019 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

"Naliagiza baraza la uuguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika,” amesema Waziri Ummy.

Aidha, amewataka watumishi  wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao.

“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili, weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za nidhamu ikiwamo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya dola," amesema Waziri Ummy.

Chanzo: mwananchi.co.tz