Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ndugulile agoma kuzindua chuo cha udaktari Musoma

11889 Ndugulile+pic TanzaniaWeb

Sun, 22 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile amegoma kuzindua chuo cha Udaktari Musoma baada ya kuhisi kuna matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho kilichopo mjini Musoma.

Badala yake, ametoa wiki mbili kwa  Mkuu wa Chuo hicho, Dominic Tarasa kuandika maelezo na mchanganuo wa matumizi ya zaidi ya Sh500 milioni zilizotumika kwenye mradi huo.

Akizungumza baada ya kutembelea chuo hicho mjini Musoma leo Julai 21, Dk Ndugulile amesema ubora wa majengo ya chuo hicho hauakisi thamani ya fedha zilizotimika kuzijenga na kuzikarabati miaka miwili iliyopita.

"Majengo yamejaa nyufa huku rangi ikionekana kupauka miaka miwili pekee ya ujenzi; Hakuna value for money (thamani ya fedha). Siwezi kushiriki uhalifu huu na lazima wahusika watoe maelezo ya kutosha," amesema Dk Ndugulile

Naibu Waziri huyo amesema matumizi ya aina hiyo yanakwamisha ufanisi katika utekelezaji wa mpango wa Serikali ya kuboresha huduma katika sekta ya afya.

Akizungumzia matumizi ya fedha na ubora wa majengo, Tarasa amesema kazi ya ujenzi na ukarabati ilisimamiwa na kuthibitishwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto.

"Ushiriki wangu katika mradi huu ulikuwa ni kupokea majengo," amesema Tarasa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz