Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu ausifu mtandao wa Aga Khan

10093 Agakhan+pic TZW

Wed, 27 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuunga mkono Mtandao wa Mashirika ya Aga Khan (AKDN) Tanzania kwa kuhakikisha wanatoa ulinzi wa mali zote walizowekeza nchini.

Akizungumza leo Juni 26 katika sherehe Jubilei ya miaka 60 ya Mtukufu Aga Khan iliyofanyika katika viwanja vya Bunge, Majaliwa amesema ni matumaini yake kuwa mtandao huo utaendelea kupanua wigo wa huduma kwa wananchi wanaohitaji huduma nchini.

“Kwetu somo muhimu ni kujitolea lakini pia kuunga mkono kwa kuwasaidia katika ulinzi wa mali wanazoziwekeza katika maeneo yote nchini kuhakikisha kuwa tunajitahidi kutumia miundombinu kupata huduma,”alisema.

Amesema jambo hilo litaendelea kuwapa moyo kwa kuona kuwa huduma wanayoitoa inahitajika na watu wao.

“Rafiki huyu wa Watanzania amekuwa na mchango mkubwa sana, katika kuinua jamii zetu kiuchumi kama ambavyo imeelezwa. Niamini kwamba wakati wote mtasimamia maslahi ya jamii yetu ili tuweze kubadilika na sisi pia,”amesema.

Amesema jumla ya wanufaika milioni mbili katika sekta ya elimu

wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mtandao huo huku katika sekta ya afya wanufaika wakiwa ni zaidi ya watu milioni 20.

Amesema mbali na kusaidia katika sekta za afya, elimu, ujasiriamali lakini hivi sasa mtandao huo umejipanga kuanzisha kiwanda cha dawa nchini.

“Aga Khan Foundation ni miongoni mwa taasisi anzilishi za hoteli

katika mbuga za kitalii, Serengeti, Ngorongoro. Ndio mtu wa kwanza kujenga hoteli za kitalii kule mbugani na sasa amesema anakwenda Ruaha, Selous. Tunashukuru kuwa ubunifu wako,” amesema.

Amesema mtandao huo pia unajihusisha na utengenezaji wa viunga vya kupumzikia, kwa upande wa Zanzibar umetengeneza kiunga cha Forodhani na kuomba kufikiria uwekezaji kama huo katika jiji la Dodoma.

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameushukuru mtandao wa AKDN kwa kuwatembelea na kwamba wabunge wamepata nafasi ya kujifunza mchango wa jamii hiyo ya Ismailia nchini.

“Tumepata nafasi ya kujifunza mchango unaofanywa na jamii hiyo,

wamewekeza katika maeneo mbalimbali ya kuimarisha uchumi lakini pia kusaidia maendeleo ya jamii ya watu,”alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa AKDN nchini, Amin Kurji aliahidi mtandao huo kufanya kazi pamoja na Serikali ya Tanzania ili kutekeleza vipaumbele vya taifa katika sekta za afya na elimu, kutengeneza ajira, kilimo, na viwanda, kutaja tu vichache.

“Tunayo mashirika tisa nchini kote ambayo kwa pamoja yanaunda AKDN, yanayofanya kazi katika sekta za afya, elimu, kupunguza umasikini, benki na fedha, utalii na kuendeleza viwanda,”amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz