Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Gwajima Kupambana na Ngo’s Korofi

GWAJIMA 2?fit=480%2C254&ssl=1 Waziri Gwajima Kupambana na Ngo’s Korofi

Wed, 12 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali haitavumilia kuona Mashirika Yasiyo ya Kiseikali yafanya kazi bila kufuata sheria.

Dkt. Gwajima amesema hayo Bungeni Jjijini Dodoma wakati kuwasilisha Hotuba ya Mwelekeo wa Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha ufuatiliaji na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yatoe mchango Chanya wa Ujenzi wa Taifa na hivyo kunufaisha Jamii. Amesema pamoja na jitihada zinazoendelea kufuatilia na kuratibu shughuli za Mashirika hayo, Serikali itahakikisha jitihada zaidi inaongeza kukomesha Mashirika yasiyotimiza masharti.

“Sitokubali kuona Shirika lolote lisilo la Kiserikali linafanya kazi bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria sitovumilia hili litokee, jisajilini mfanye kazi kwa utaratibu” Waziri Gwajima. Amesema shilingi milioni 585.5 zimetengwa kwa aliji ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 1,000 Tanzania Bara.

Waziri Gwajima pia amezungumzia umuhimu wa kukuza Uzalendo wananchi na ari ya kujitolea kujiletea Maendeleo yao kwa kutumia rasrimali zinazowazunguka ambapo shilingi milioni 350.7 zimetengwa kufanikisha azma hiyo. Aidha amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia na kuhakikisha wanawake wamepata nafasi zaidi za uongozi na maamuzi.

Akizungumzia umuhimu wa makundi maalum katika Jamii wakiwemo watoto, wazee na wenye ulemavu, Mhe. Gwajima amesema Serikali itaaendelea kuboresha huduma za Ustawi wa Jamii, kuboresha huduma kwa Wazee, kufuatilia na kuimarisha uanzishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo na kuboresha huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa na familia.

“Niseme jumla ya Shilingi bilioni 12.4 zimetengwa kwa ajili hiyo ikiwemo kukarabati majengo na miundombinu katika makazi 10 ya wazee ili kuwezesha kuwa na amzingira mazuri ya kulea wazee na wasiojiweza,” Waziri Gwajima.

Waziri Gwajima amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kuratibu kampeni mbalimbali za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Jumla ya Shilingi milioni 791 zimetengwa kwa ajili ya kuratibu kampeni za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Chanzo: globalpublishers.co.tz