Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Bashungwa kuzindua wiki ya magonjwa yasiyoambukiza

Bashungwa12 innocent Bashungwa, Waziri wa Saana na Utamaduni

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa kesho Oktoba 6, 2021 anatarajiwa kuzindua maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yatakayofanyika Kitaifa mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani humo kuanza Oktoba 6 hadi 13, mwaka huu.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo; ‘Badili mtindo wa maisha boresha afya,’ yamelenga juhudi za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la damu, kisukari na saratani.

Amesema katika maadhimisho hayo kutafanyika mambo mbalimbali ikiwemo huduma za upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza na ajenda nyingine ikiwemo ya michezo.

"Niwaombe wana Arusha tujitokeze kwa wingi katika maadhimisho haya ili tuweze kupata elimu mbalimbali za masuala ya afya ikiwemo upimaji, ajenda za michezo na tushirikiane kwa pamoja kufanikisha maadhimisho haya.

"Takwimu za kidunia zinaonyesha zaidi ya asilimia 71 ya vifo vyote duniani vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo mwaka 2016 zinaonyesha watu milioni 57 duniani walipoteza maisha kutokana na magonjwa hayo," amesema.

Chanzo: mwananchidigital