Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee walia na ukosefu wa dawa

5788 WAZEE Dawa TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

LICHA ya huduma ya afya kuwa bure kwa wazee nchini hali imekuwa tofauti kwa wazee wasiojiweza katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa kukosa dawa katika hospitali wanazotibiwa, hali inayowalazimu kwenda kununua kwenye maduka binafsi.

Akizungumzia changamoto hiyo Kaimu Msaidizi wa Makazi ya Wazee katika kituo cha Njoro, Josephine Kessy alisema mara nyingi imemlazimu kutoa fedha zake binafsi na kuwasaidia wazee katika kituo hicho kwenda kununua dawa katika maduka binafsi kwa vile hospitalini walikotibiwa dawa hazipo. Kessy alisema hayo baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa walimu wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya Mecson ya Jijini Arusha ambapo alisema wazee hao wanapougua hupatiwa huduma ya kumuona daktari na vipimo bure ila changamoto inatokea kwenye upande wa dawa.

“Wakati mwingine inanilazimu mimi msimamizi wa kituo kutoa pesa yangu ya mfukoni kuwanunulia dawa wazee hawa kwani wapo kwenye kituo na hakuna fungu kwa ajili hiyo,” alisema Kessy. Wakizungumza kuhusu adha hiyo, mwenyekiti wa wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo hicho, Enyasi Athanas alisema wanapata magonjwa mbalimbali yanayowadhoofisha na pindi wanapokwenda kwenye vituo vya afya na hospitali hupatiwa tiba ila dawa zinakosekana. Akizungumzia msaada huo, Meneja wa Shule hiyo, Ernst Shirima alisema wameguswa kuwasaidia wazee hao baada ya kuona wengi wao wamesahaulika katika jamii na hivyo kuwa wapweke.

Chanzo: habarileo.co.tz