Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi wakumbushwa malezi mema kwa watoto

Ad453c619f16085906bcd4da9b13caf3 Wazazi wakumbushwa malezi mema kwa watoto

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dk John Jingu amekemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi mkoani Rukwa kuwashawishi watoto wao kuandika majawabu ya uongo ili wafeli mitihani yao ya Kitaifa.

Alisema hayo wakati akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto yaliyofanyika juzi katika mji mdogo wa Laela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa katika ngazi ya mkoa. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Dunia Yenye Usawa wa Kila Mtoto Inawezekana.’

Aliwataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa kuwalea watoto wao kwa kuzingatia maadili badala ya kuwatelekeza bila usimamizi na kujikita katika shughuli za kuwaongezea kipato na kusababisha wajiingize katika matendo maovu.

"Wazazi na walezi timizeni wajibu wenu kwani jukumu la malezi bora ni letu sote ...tusipotimiza tunatengeneza jamii isiyo na maadili na uzalendo. Pia watoto ni wajibu wenu kuwaheshimu wazazi walezi na walimu wenu pia kusoma kwa bidii" alisisitiza.

Katika risala ya watoto wa mkoa wa Rukwa, walishukuru serikali ya Awamu ya Tatu kwa kutekeleza Sera yake ya Elimu Bila Malipo pia kuendelea kupambana na visa vya ukatili dhidi yao.

Chanzo: habarileo.co.tz