Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazawa Mloganzila wafanya upasuaji wa kupunguza uzito kwa matundu madogo

Wazawa Mloganzila Wafanya Upasuaji Wa Kupunguza Uzito Kwa Matundu Madogo Wazawa Mloganzila wafanya upasuaji wa kupunguza uzito kwa matundu madogo

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kutumia madaktari wazawa kwa mara ya kwanza imefanya huduma ya ubingwa bobezi ya kupunguza uzito kwa kutumia matundu madogo kwa watu wenye uzito uliopitiliza kwa mtu mwenye kilo 145.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji MNH-Mloganzila, Dkt. Edwin Muhondezi huduma hiyo imehusisha kupunguza sehemu ya tumbo ambapo kwa kufanya hivyo itamfanya mtu atumie chakula kidogo ukilinganisha na awali hatua itakayomuwezesha apunguze uzito.

“Huduma hizi hapo awali zilikuwa zinafanyika nje ya nchi kwa gharama kubwa ambapo kwa kuzifanya hapa Mloganzila zinafanyika kwa gharama nafuu zaidi na kupunguza usumbufu waliokuwa wakiupata kutafuta huduma hizo nje ya nchi na pia kutawavutia watu wengine kutoka mataifa ya jirani kuja kupata huduma hivyo kuongeza pata la nchi” ameongeza Dkt. Muhondezi

Dkt. Muhondezi ameongeza kuwa huduma hizi za ubingwa bobezi zimewezekana kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali ambao umehusisha katika uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma, kuwajengea uwezo wa wataalam na uwepo wa vifaa tiba vya kisasa.

Aidha, Dkt. Muhondezi ameishauri jamii iendeleze utaratibu wa kufanya mazoezi na kuzigatia taratibu bora za lishe ili kuepuka uzito uliopitiliza ambao unaweza kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, pamoja na magonjwa ya kiharusi.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imekuwa ikifanya huduma mbalimbali za ubingwa bobezi ikiwemo ya kupunguza uzito kwa kutumia puto maalum (intragastic balloon), kuondoa uvimbe kwenye skafu ya ubongo kwa kutumia matundu ya pua, kupandikiza figo na kuondoa mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mtetemo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live