Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili kupandikizwa figo Hospitali ya Mkapa

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Hospitali ya Benjamin Mkapa Ultra Modern iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma, leo Jumatano Agosti 29, 2018 itaendelea na upandikizaji wa figo kwa wagonjwa wawili.

Akizungumza na MCL Digital leo mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Alfonce Chandika amesema katika awamu hii ya pili jumla ya wagonjwa watatu walipangwa na tayari mgonjwa mmoja alihudumiwa jana.

Dk Chandika amesema huduma hiyo ambayo ilianza kutolewa Machi 20 mwaka huu, inatarajia kuboreshwa zaidi ikiwemo kuongeza idadi ya wagonjwa wanaotibiwa.

"Sambamba na hilo, tumeamua kupeleka madaktari wawili nchini Japan ambao watajifunza kwa muda wa miezi sita na wakirudi watakuwa wazuri hata kuwafundisha na wengine," amesema Chandika.

Amesema huduma hiyo itakuwa ikitolewa kila baada ya miezi mitatu kwa idadi ya watakaojitokeza.

Machi 2018, hospitali hiyo ilianza kutoa huduma ya kwanza ya kupandikiza figo.

Chanzo: mwananchi.co.tz