Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wauguzi, Wakunga, wataka waongezwe

C2690e99ea1744e25e0a8c6c998ec3f7 Wauguzi, Wakunga, wataka waongezwe

Mon, 18 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Wauguzi na Wakunga nchini(TANNA) kimesema sekta ya afya nchini inakabiliwa na upungufu wa wauguzi na wakunga, hivyo muuguzi mmoja analazika kuwahudumia wagonjwa kati ya 50 na 60 kwa siku, badala ya wagonjwa nane.

Hivyo kimeiomba serikali kama ilivyoajiri madaktari 1,000 na walimu zaidi ya 10,000 basi ifanye hivyo kwa wauguzi na wakunga ambao wamehitimu masomo yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini hapa, Makamu wa Rais wa TANNA, Ramadhan Mgoo alisema alisema sekta ya afya nchini inakabiliwa na upungufu wa wauguzi na wakunga ambapo waliopo ni chini ya asilimia 50 ya mahitaji halisi.

Chanzo: habarileo.co.tz