Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu zaidi ya milioni 92 wamepewa chanjo ya COVID-19

New New Repoty Maambukizi ya Corona yapungua Afrika

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Corona kwa nchini 55 za barani Afrika ni milioni 8,339,974 huku jumla ya idadi ya waliopokea chanjo ni 92,936,756.

Ripoti hii imetolewa leo Oktoba 4, 2021 na Shirika la Afya la barani humu, na kubainisha kuwa jumla ya idadi ya vifo ni 212,056 na idadi ya waliopona ugonjwa huu ni 7,632,069.

Hata hivyo ripoti hii imeonesha kuwa nchi ya Afrika Kusini inaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi yaliyofika 2,906,422 huku jumla ya vifo vikiwa ni 87,780.

Nchi nyingine ambazo zimeathirika na janga hili ni Morocco yenye maambukizi 935,332, Tunisia 708,203, Ethiopia 348,669, Libya 341,839, Egypt 306,798 na kenya 250,114.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live