Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu zaidi ya 800,000 wachanjwa chanjo ya Uviko-19

CHANJO ED (1) Watu zaidi ya 800,000 wachanjwa chanjo ya Uviko-19

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi amesema zaidi ya watu 850,000 wameshapata chanjo ya Uviko-19 mpaka kufikia Oktoba 9, 2021 nchini kote.

Profesa Makubi amesema hayo leo Jumapili Oktoba 10, 2021 wakati akihamasisha waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Katoliki Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya jamii harakishi na shirikishi inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi).

Amesema kupitia kampeni hiyo watu wengi wameelimishwa na kupata uelewa wa chanjo na kuondoa zile sintofahamu ambazo zilikuwa zinaleta hofu katika jamii.

Akihutubia waumini kanisani, Profesa Makubi amesema chanjo za Uviko-19 zilizoletwa nchini ni salama kwa kuwa zimethibitishwa na wataalamu na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Profesa Makubi amesema mwitikio wa wananchi kujitokeza kupata chanjo baada ya kuanzishwa kampeni ni mkubwa na baada ya kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan idadi ya waliochanjwa ilikuwa 28,000 nchi nzima lakini baada ya kampeni mpya ya jamii shirikishi, watu zaidi ya 850,000 wamechanjwa mpaka jana.

Profesa Makubi amesema kampeni ya jamii harakishi na shirikishi ilizinduliwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kuchanja katika maeneo mbalimbali ikiwamo makanisa, misikiti, makundi mengine kama wanamichezo, makazini, masokoni, kwenye kaya na sehemu zote zenye mikusanyiko kuanzia mijini mpaka vijijini.

Chanzo: mwananchidigital