Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu zaidi ya 7,000 wagundulika kuwa na TB

C016ed5c667b93466558372e5f9e5ba7.png Watu zaidi ya 7,000 wagundulika kuwa na TB

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WIZARA ya Afya imesema watu 7,215 wamebainika kuugua kifua kikuu (TB) mwaka jana.

Takwimu hizo zilitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani, ambapo wizara hiyo imesema programu ya kupambana na ugonjwa huo nchini mwaka jana ilibaini watu idadi ya watu hao waliugua ugonjwa huo mwaka jana.

Ilisema maadhimisho ya siku hiyo ni fursa kwa mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine kukumbuka jukumu lao la mapambano dhidi ya kifua kikuu ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na wizara hiyo, ugonjwa huu ni moja wapo ya vikwazo vikubwa vya maendeleo endelevu nchini na Afrika kwa ujumla.

Wizara hiyo imetoa wito mtu yeyote aliye na kikohozi sugu kupima na kupata matibabu kabla ya kuwaambukiza wengine.

“Kumbuka kuwa kikohozi kinachozidi wiki mbili, joto, jasho la usiku na asthenia ni dalilia kubwa ya kusumbuliwa na ishara za dalili za kifua kikuu,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, takribani watu 2,800 wanapimwa kifua kikuu kila siku na zaidi ya 4,000 hufa kutokana na ugonjwa huo kila siku.

Chanzo: www.habarileo.co.tz