Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu milioni 1.2 wamepata chanjo ya Corona

0be08989 002b 401e A0c1 A2b19bedb6ee Corona World 4a321e62 586x394 478x394 Watu 1.2 milioni wachanjwa chanjo ya Corona

Sun, 19 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania imesema hadi kufikia Desemba 18,2021 watu zaidi ya 1.2 milioni wamechanjwa na kupata kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19.

 Hayo yamesemwa leo Jumapili Desemba 19,2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi.

Amesema lengo ni kufikia asilimia 60 ya wananchi wote ambayo ni sawa na watu milioni 35.

Profesa Makubi amesema mwitikio wa watu kuchanja sio wa kusuasua ukilinganisha na nchi nyingine.

Amesema kilichochangia watu wengi kutojitokeza ni taarifa potofu zilizoanza kutolewa na makundi mbalimbali ya kijamii kuhusu chanjo hiyo wakati suala la chanjo lipo nchini kwa zaidi ya miaka 100 sasa. “Imetuchukua muda kuwaelimisha wananchi ili tuwaondolee hayo mashaka. Natumaini sasa wananchi wametuelewa, elimu inatolewa na kesho yake wanachanja,”amesema.

Aidha, Profesa Makubi amesema Desemba 22,2021 watafanya uzinduzi wa kampeni-jamii shirikishi ya pili dhidi ya afua na kinga ya Uviko-19 jijini Arusha.

Advertisement Amesema ili kufanikisha malengo ya awamu ya pili na matumizi ya watoa huduma ngazi ya jamii, Wizara na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeandaa mwongozo wa wawezeshaji wa wahudumu wa afya ya jamii. Mwisho

Chanzo: www.tanzaniaweb.live