Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 800 wafariki kwa Corona nchini

CORONA DUNIANI IMICRON Watu 800 wafariki kwa Corona nchini

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watanzania 800 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa Covid-19 tangu kuingia kwa virusi vya ugonjwa huo, corona miaka miwili iliyopita.

Msemaji wa serikali, Gerson Msigwa amesema ugonjwa huo bado upo nchini humo na unaendelea kuathiri mamia ya watu.

'Uviko (Corona) bado upo Tanzania', alisema Msigwa na kusisitiza watu kuchukua tahadhari ikiwemo kuchanjwa, 'sasa hivi mchawi ni chanjo, msifanye masihara ndugu zanghu twendeni tukapate chanjo, watu wanaumwa na watu wanapoteza maisha'.

Mpaka sasa Tanzania imepokea chanjo 11.2 milioni, kati ya hizo chanjo milioni 8.4 zimeshatumika.

Zaidi ya watu nusu bilioni wameambukizwa virusi vya Corona na kuua watu zaidi ya 6.3 milioni duniani kote,

Chanzo: www.tanzaniaweb.live