Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 519 watajwa kuugua kipindupindu, 11 wafariki dunia

Kipindupindu Vifo Watu 519 watajwa kuugua kipindupindu, 11 wafariki dunia

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takwimu za Wagonjwa wa Kipindupindu Nchini Tanzania kuanzia Januari 2022 hadi Agosti 2022 ni visa 519 ambapo kati yao 11 wamefariki Dunia, Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ikitajwa kutoa wagonjwa wengi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia sheria za usafi wa mazingira ili kudhibiti na kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo.

“Kipindupindu ni Ugonjwa wa masikini, na unaendezwa kwa njia kubwa mbili ambazo ni maji au chakula kisicho salama.

“Aidha, takwimu zinaonesha Afrika inachangia 20% ya maambukizi ya ugonjwa huo Duniani, pia inachangia 80% ya vifo vya Kipindupindu,” – Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live