Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 5 kati ya 10 wana shambulio la moyo

Heart Attack Ms.jpeg Watu 5 kati ya 10 wana shambulio la moyo

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Palangyo, amesema kati ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kufanya uchunguzi, asilimia 50 hukutwa na changamoto ya dalili ya shambulio la moyo kutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye moyo.

Shambulio la moyo (heart attack) husababishwa na kuziba kwa mishipa inayopeleka damu kwenye moyo. Ugonjwa huo unaweza kusababisha kusimama kwa moyo yaani ‘cardiac arrest’.

Wataalamu wanaeleza dalili za ugonjwa huo ikiwa ni Maumivu ya kifua Maumivu katika sehemu zingine za Kuhisi kizunguzungu Kutokwa na jasho, upungufu wa pumzi, wasiwasi, kukohoa au kupumua kwa shida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live