Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 494 wanaoishi na VVU Mwanza, wanatumia dawa za ARV

Watu 494 Wanaoishi Na VVU Mwanza, Wanatumia Dawa Za ARV Watu 494 wanaoishi na VVU Mwanza, wanatumia dawa za ARV

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza,Dk. Alice Kaiajege imelishukuru Shirika la ICAP kuleta vifaa Mwanza kuisaidia serikali kutimiza lengo la kuboresha afya za Watanzania na kupata ajira na kipato kupitia miradi ya shirika hilo.

Ametoa shukurani hizo leo baada ya kupokea taarifa fupi ya mradi wa utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS 2022-23) na FIKIA+ na kuishauri serikali kuongeza nguvu katika eneo la kutoa elimu kuhusu ugonjwa Ukimwi ili kuifanya jamii iwe na uelewa mpana na hivyo ishirikiane na ICAP kuwaunganisha wasichana barehe na SIDO ili wafanye shughuli za ujasiriamali. Makamu Mwenyekiti

Awali, Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoani Mwanza, Dk.Pius Masele akitoa takwimu kwa wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kwa niaba ya MgangaMkuu wa Mkoa huo, Dk.Thomas Rutachunzibwa amesema watu 4,494 kati ya 4,515 waligundulika kuwa na VVU kutoka miongoni mwa watu 93,108waliopata huduma ya kupima VVU kupitia mradi wa FIKIA+ katika kipindi cha Julaihadi Septemba 2022.

Amesema asilimia 99.5 ya watu hao 4,494 kati ya 4,515 waligundulika baada ya huduma na ICAP na wanapata huduma za tiba na matunzo .

Dk.Masele amesema pia ICAP inatoa huduma za uchunguzi wa Kifua Kikuu(TB) na takwimu za Septemba 2022 mwishoni zinaonyesha watu 117,717 walichunguzwa kifua kikuu, kati yao 2,310 walihisiwa na 519 walianza tiba baada kugundulikawana TB ambapo Mwanza ina jumla watu 118,164 wanaoishi na VVU.

“Vifaa vya kisasa vya geneExpet ndivyo vinavyotumika kupima TB na watu8,616 wanaoishi na VVU ili kuwakinga na ugonjwa huo walianzishiwa dawa kinga yaIsoniazid (IPT),nawashukuru ICA na PEPFAR kwa kuendelea kuishika serikali mkono katika utambuzi wa maambukizi mapya ya VVU,”amesema.

Mratibu huyo wa Ukimwi mkoani humu amesema wanahakikishawatu wenye VVU wanaanzishiwa dawa za kufubaza, kuimarisha mwendelezo wamatibabu na kufubaza virusi miongoni mwao,wameimarisha huduma za kuzuiamaambukizi mapya kwa tohara kinga kwa wanaume, tiba kinga kwa mabinti rika barehena wanawake vijana (DREAMS).

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Programu wa ICAP nchini, Dk. John Kahemele amesemawanafanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS 2022-2023) kwasampuli ya watu 40,000 wa umri wa miaka 15 na zaidi kutoka kaya 19,000 Tanzania Bara na Visiwani ili kuhakikishautambuzi wa maambukizi mapya ya VVU unakuwa endelevu.

"Tunapambana kuhakikisha huduma za tiba zinakuwa bora katika vituovyetu na lengo la utafiti ni kubainiwaathirika ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU,hivyo tunawaomba wananchi kujitokezana kutoa ushirikiano kwa watalaam wetu waweze kufahamu afya zao na kuchukuahatua," amesema Dk.Kahemele.

Mkuu wa Kitengo cha Kinga, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP)Evaline Maziku alisema huduma za kujipima kwa kutumia vitepe mkoa wa Mwanzaumefanya vizuri hivyo 95-95-95 itashuka kwa kuhusisha sekta mbalimbali zinazotoahuduma za Ukimwi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live