Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto zaidi ya 6,000 huzaliwa na VVU kwa mwaka

Watoto VVU Wizara ya Afya yatoa tamko kukithiri kwa idadi ya maambukizi ya VVVU kwa watoto

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wajawazito wote nchini kuhakikisha wanahudhuria katika vituo vya afya kwaajili ya kufanya vipimo mbali mbali vya kiafya ili kuweza kuwakinga watoto wao.

Ametoa rai hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa 'twitter' na kuwataka wanawake hao kuhakikisha wanapata vipimo vya VVU kufuatia kukithiri kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi hivyo.

Waziri Ummy amesema kuwa zaidi ya watoto 6,000 nchini huzaliwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI idadi aliyoitaja kuwa ni kwa mwaka mmoja pekee.

"Je unajua?? Zaidi ya watoto 6,000 nchini Tanzania huzaliwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa mwaka. Lengo ni kuona hakuna mtoto anazaliwa na VVU nchini. Ninahimiza wanawake wajawazito kwenda clinic, kupima na kwa wale wenye maambukizi ya VVU tutawapa Dawa ili kuwakinga watoto wao. Ameandika Waziri huyo.

Hata hivyo mapema Januari 20, 2022 Wizara ya Afya ilitangaza kuwatafuta watanzania zaidi ya 200,000 waishio na maambukizi ya virusi hivy ambao hawafahamu kama wameambukizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live