Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto watano wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Arusha

Vifo Ajabu Arusha Watoto watano wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Arusha

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto watano wa familia moja wakazi wa kijiji cha Mswakini wilayani Monduli, mkoa wa Arusha, wamefariki dunia kwa ugonjwa ambao bado haujatambulika baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo na tumbo kujaa.

Diwani wa Kijiji cha Mswakini, Nanga Lenasira Mollel amesema vifo vya watoto hao vimetokea kwa nyakati tofauti kuanzia Julai 5 hadi Julai 19 ambapo amefariki mtoto mwingine aliyekuwa amebakia katika hospitali ya Mount Meru Arusha.

Amesema mtoto wa kwanza, Bosi Nyangusi alifariki Julai 5, 2022 kutokana na kusumbuliwa na tumbo, na baadaye wanzake wanne walipelekwa hospitali ya TMA Monduli kwa ajili ya matibabu kisha wakaruhusiwa. Wakati wakiwa njiani walizidiwa na kupelekwa Mout Meru, ambapo Julai 16 alifariki Saimalie.

Ameongeza kuwa, baadaye watoto wawili walifariki Julai 17 ambao ni Lemali na Sophia, huku aliyekuwa amebaki amelazwa hospitali ya Mount Meru, Veronica aliyekuwa anasoma darasa la tatu Mswakini kufariki leo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mswakini, Nanga Karani amesema wamekuwa wakifuatilia chanzo cha vifo hivyo bila mafanikio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live