Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanaougua saratani Muhimbili wapewa msaada wa Mil. 15

Watoto Wanaougua Saratani Muhimbili Wapewa Msaada Wa Mil. 15.jpeg Watoto wanaougua saratani Muhimbili wapewa msaada wa Mil. 15

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lions Club International wametoa msaada wa dawa zenye thamani TZS 15 Mil kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaogua saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema serikali imechukuwa nafasi kubwa kwenye matibabu ya watoto wanaougua saratani kwani matibabu yao ni gharama na yanachukuwa mda mrefu.

“Tunashukuru kwa msaada huu pia tunawakaribisha wadau wengine kuja kusaidia Hospitali yetu ya Taifa kwani uhitaji ni mkubwa kulingana na idadi ya wagonjwa”amesema Prof. Janabi.

Kwa upande wake, Bw. Mustansir Gulamhussein ( District Governor) amesema wameguswa kuja kutoa msaada wa dawa kwa watoto wenye saratani ikiwa ni malengo yao ambayo wamejiwekea.

“Swala la afya ni kipaumbele chetu sisi kama Lions Club International watoto ndio taifa la kesho hivyo ni jukumu letu kuwasaidia” amesema Bw. Mustansir.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live