Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto njiti 9500 hufariki kila mwaka -Dkt. Mpango

Mpango.png Philips Mpango, Makamu wa Rais

Sun, 14 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wa maendeleo ikiwemo kampuni ya DataVision International wametakiwa kuelekeza juhudi katika kuelimisha jamii juuya umuhimu wa Lishe na afya ya uzazi ili kupunguza matatizo yanayotokea kwenye jamii kutokana na kukosa elimu hizo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango ametoa wito huo katika hitimisho la mbio za hisani za CRDB zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kuna tatizo kubwa la watoto wanaozaliwa kabla ya umri wao ambapo watoto njiti 9500 hufariki kila mwaka baada ya kuzaliwa.

Amesema Kila mwaka watoto njiti laki 2 huzaliwa kutokana na sababu tofauti ikiwemo wajawazito kubeba mimba za mapacha, Magonjwa ambukizi na magonjwa ya muda mrefu kama kisukari na magonjwa ya damu.

“Hapa nchini Watoto laki mbili huzaliwa kabla ya wakati kwa mwaka, na kati ya hao takribani watoto 9500 hufariki muda mfupi baada ya kuzaliwa, hii ni sawa na asilimia 4.75% ya watoto wote wanaozaliwa kabla ya wakati na hili jambo halikubaliki,” amesema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa, “Serikali inaendelea kuboresha huduma za watoto njiti lakini bado kuna upungufu wa vifaa tiba kwa watoto hawa, hivyo nawaomba muwekeze katika kuisaidia serikali katika kutoa huduma bora na pia muongeze huduma za kutoa elimu kwa masuala ya afya ya uzazi.”

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa tukio hilo ambao wamefanya kazi ya kutoa huduma ya kwanza eneo la tukio bwan Obadiah Salim wa Emergency Plus Medical Services ameiomba serikali kusogeza huduma hizo kwa jamii ili kupunguza matatizo ya vifo vya watoto wenye magonjwa ya moyo.

Mbio za hisani za CRDB zimekuwa zikifanyika kwa miaka 3 mfululizo zikishirikiana na makampuni ya kijamii kama Datavision International ili kusaidia watoto wenye matatizo ya Moyo katika hospitali ya JKCI, na wanawake wenye ujauzito hatarishi katika hospitali ya CCBRT.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live