Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto nane wafariki kwa surua Zanzibar

Image 125.png Watoto nane wafariki kwa surua Zanzibar

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: Dar24

Zaidi ya watoto 1,742 wenye umri chini ya miaka 15 wameugua surua na wanane kati yao kufariki kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2022 ambapo wazazi na walezi wamehimizwa kuwapeleka watoto wanaopaswa kuchanjwa na kupatiwa matone ya Vitamin A ili kutokomeza maradhi hayo yanayoweza kusababisha upofu, kupooza na hata kifo.

Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 18, 2022 na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman katika eneo la Masingini Wilaya ya Magharib A wakati akizindua Chanjo ya Surua, Polio na utoaji wa matone ya Vatamin A, kwa watoto ili kuzuia na kudhibiti mripuko wa maradhi hayo.

Amesema, hatua hiyo ya kuendesha kampeni ya chanjo inatokana na uwepo wa maradhi hayo tangu Januari na mwezi Machi 2022 ambapo jumla ya wagonjwa 17,500 waliripotiwa katika visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba watahakikisha wanazuia uingiaji wa Ugonjwa wa Polio kama ilivyotokea kwa nchi za Msumbiji na Malawi.

“Wataalamu wa wizara ya Afya watahakikisha kupita nyumba kwa nyumba katika kampeni hiyo ili kuwachanja na kuwapatia matone ya vitamin A watoto wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 350,000 katika visiwa vya Unguja na Pemba na Serikali inafanya hivi kwa kutambua kwamba kinga ni bora kuliko tiba,” amesema Othman.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazuri suala la utoaji wa chanjo mbali mbali liliyumba mwaka 2020 baada ya kuzuka maradhi ya Uviko-19 na kwamba baada ya kudhibitiwa ugonjwa huo nguvu kubwa inaelekezwa katika chanzo za surua, Polio na utoaji wa matoni ya Vitamin A.

Awali, Mtalamu wa Chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Wilium Mwenge amesema kwamba Mashirika na wadau mbalimbali wa Afya Duniani , wanaunga mkono juhudi za serikali za na kwamba kwa pamoja wataendelea kutoa ushirikiano katika jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.

Chanzo: Dar24