Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto Pacha waliofanyiwa upasuaji Saud Arabia kutua Tanzania

73489 Saudi+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watoto pacha Anisia na Merynes Bernad waliozaliwa wilayani Misenyi mkoani Kagera nchini Tanzania wakiwa wameungana wanatarajiwa kuwasili nchini humo leo Ijumaa Agosti 30,2019 baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha nchini Saudi Arabia.

Pacha hao walizaliwa Januari 29, 2018 katika Kituo cha Masista cha zahanati ya St. Theresa Omukajunguti, Kyaka Misenyi. Walisafirishwa hadi hospitali ya kanda ya Bukoba kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.

Walipelekwa Saud Arabia Julai 8, mwaka 2018 baada ya Mfalme Salman kutoa idhini ya kufanyika kwa upasuaji huo kwa gharama ya Serikali ya Saudia.

Shughuli ya upasuaji wa pacha hao ulichukua saa 13  huku ukiwahusisha madaktari bingwa na wataalamu wengine 32 huku upasuaji huo ulielezwa kufanyika kwa mafanikio makubwa.

Dk Abdullah Al-Rabeeah wa Hospitali ya King Abdullah Children’s Specialist ya Riyadh aliyeongoza jopo hilo la watu 32 alinukuliwa na mtandao wa saudigazette.com.sa Desemba 2018 akisema upasuaji huo ulifanyika vizuri.

Pacha hao waliungana kutoka kwenye koo, tumbo, mfupa wa nyonga, miguu mitatu lakini kila mmoja ana moyo wake.

Pia Soma

Advertisement     ?
Kabla ya kupelekwa Saudia Arabia pacha hao walikuwa wakihudumiwa na madaktari katika hospitali ya MNH.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Alhamisi na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha pacha hao watawasili saa 08:40 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3 kwa ndege ya Shirika la Emirates EK 816.

Alisema watoto hawa watasafirishwa kwenda nyumbani kwao Misenyi mkoani Kagera Septemba 6, 2019.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz