Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 58,719 Mbogwe kuchanjwa Rubella, Surua

Thumb 598 800x420 0 0 Auto Watoto 58,719 Mbogwe kuchanjwa Rubella, Surua

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watoto 58,719 wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya magonjwa ya Surua na Rubella, huku wazazi wao wakisisitizwa kuwapeleka kupata huduma hiyo.

Wilayani Mbogwe, huduma hiyo imeanza kutolewa leo Februari 15 2024 na itaendelea hadi Februari 18, mwaka huu.

Taarifa kuhusu chanjo kwa watoto hao, imetolewa leo Alhamisi, Februari 15, 2024 na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Dk Jacob Rombo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.

Dk Rombo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wanaostahili kupata chanjo hiyo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa hayo.

“Chanjo ya Surua na Rubella hutolewa kwa awamu mbili; awamu ya kwanza inatolewa kwa mtoto anapotimiza umri wa miezi tisa na awamu ya pili hutolewa kwa mtoto baada ya kutimiza miezi 18,” amesema DK Rombo.

Hadi kupatikana kwa chanjo hizo, Dk Rombo amesema Serikali imetumia fedha nyingi, kuigharimia kutokana na umuhimu wake kwa watoto.

“Chanzo hii inawakinga watoto tangu wakiwa wadogo na magonjwa kama Surua na Rubella, magonjwa haya yanaathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara kama upofu, uziwi na hata kusababisha kifo,” amesema Dk Rombo.

Amesema ni muhimu wazazi wakapeleka watoto wote ili kutimiza lengo la Serikali la kuwachanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live