Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 4,000 wana kisukari Tanzania

Kisukari 640x400 Watoto 4,000 wana kisukari Tanzania

Mon, 16 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Imebainika kuwa watu wengi wanaishi na ugonjwa wa sukari bila kujijua, hivyo wataalamu wameshauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili waweze kukabili ugonjwa huo.

Aidha,  rekodi za Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA), zinaonesha zaidi ya watoto 4,000 wanaishi na kisukari huku kikitaja ugonjwa huo kuwa ni tatizo kubwa kutokana na idadi ya watu kuongezeka.

Meneja wa TDA, Happy Nchimbi amesema  ili kupata takwimu hizo, chama kimekuwa kikiangalia vituo au kliniki ambazo zipo kwenye hospitali za mikoa zilizoanzishwa kwa jitihada za chama kusaidia watoto baada ya kugundulika kwamba wao pia wanapata kisukari.

Via: Habarileo

MTOTO STAA MWENYE MIAKA 10 AMJENGEA MAMA YAKE NYUMBA YA KIFAHARI YA MAMILIONI, ITAZAME HAPA

Chanzo: millardayo.com