Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 30 wafanyiwa upasuaji wa moyo JKCI

Watoto 30 Wafanyiwa Upasuaji Wa Moyo JKCI.png Watoto 30 wafanyiwa upasuaji wa moyo JKCI

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya watoto 30 wamefanyiwa upasuaji wa moyo kati ya watoto 50 waliofanyiwa uchunguzi katika kambi ya siku 10 iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI,Dk Tatizo Waane amesema kambi hiyo imefanywa na madaktari kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI.

"Huu ugeni umekuwa ukija mara kwa mara matibabu hayo ni muhimu yanaokoa gharama timu hii ya wataalamu kwa kushirikiana na wataalamu wa JKCI wameweza kuchangi Sh bilioni 4.5 toka walipoanza matibabu haya miaka mitano sasa.

Amesema kwasasa wataalamu hao wametoa matibabu ya Sh milioni 700 kwa watoto hao 30 waliofanyiwa upasuaji wa moyo.

Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Yahya Okeish aliwashukuru madkatari na timu yote kutoka kituo cha King Salman na madkatari wa JKCI kwa kufanikisha matibabu ya watoto hao.

"Ninaona heshima kushiriki nanyi kuhitimisha kambi hii ya matibabu ya moyo huu ni ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia na tunapata faida hasa kwa watu tunafurahi naamini kuwaona tena wakitembelea Tanzania tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live