Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 25 kufanyiwa upasuaji presha ya macho

C54ae6513dc13f40fdec6f23ce6a639a Watoto 25 kufanyiwa upasuaji presha ya macho

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto 25 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho, makengeza na presha ya macho.

Hayo yalisemwa na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (TOS), ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya macho katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dk. Christopher Mwanansao, wakati wa uzinduzi wa wiki ya ugonjwa wa shinikizo la Macho.

Amesema huduma ya upasuaji wa watoto hao, ilianza Jumatatu na inatarajia kumalizika ndani ya siku saba.

Dk. Mwanansao alisema ugonjwa wa shinikizo la macho ni kundi la magonjwa ya macho yanashambulia mshipa wa ufahamu unaopeleka mawasiliano ya kuona kwenye ubongo.

Amesema ugonjwa huo unasababishwa na presha ya macho kuwa juu, kutokana na hitilafu katika mzunguko wa maji kunakosababisha uharibifu wa mshipa wa fahamu, hivyo mtu kupoteza uwezo wa kuona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live