Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 15 wenye vichwa vikubwa kuwafanyia upasuaji MOI

63501 Moipic

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi) nchini Tanzania imewafanyia upasuaji jumla ya watoto 15 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Akizungumza hayo leo Jumatano Juni 19, 2019 Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Respicius Boniface wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma, amesema wanawafanyia watoto hao upasuaji huo leo kwa kuwa wapo wengi wasiendelee kukaa kwa muda mrefu.

Dk Boniface amesema watawafanyia watoto 15 na kufikia mwisho wa wiki hii Taasisi ya Moi itakuwa imewafanyia upasuaji huo jumla ya watoto 60.

Amesema wakati wanaendelea na upasuaji kwa watoto hao huku watu wazima na wao wataendelea kufanyiwa upasuaji kama kawaida.

“Kwa mwezi tunawafanyia upasuaji watoto 100 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi na inapofika mwisho wa mwaka tunafanya upasuaji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi watoto kati ya 3,000 hadi 4,000 ambapo kila siku tunawafanyia watoto watatu,” amesema Dk Boniface.

Daktari Bingwa wa Upasuaji, Magonjwa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Hamis Shabani amesema wazazi wanawaleta watoto hao wakati ugonjwa ushakuwa mkubwa hivyo tunaomba wawalete wiki ya kwanza wanapoona dalili za ugonjwa huo.

Pia Soma

“Changamoto iliyopo tukishawatibia hawa watoto na tukiwapa nauli ya kuondoka nyumbani wazazi wao hawarudi na hatujui kama wamekufa au wazima na tumeshawatibia Zaidi ya 1000 lakini wanaokuja kliniki hawazidi 200 ambao ni wachache ambapo tunataka tuwaone ili tuendelee kutoa ushauri,” amesema Dk Shabani.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz