Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 12 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa surua Tanzania

Watoto 12 Wapoteza Maisha Kutokana Na Ugonjwa Wa Surua Tanzani Watoto 12 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa surua Tanzania

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Watoto 12 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na surua katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi kusini magharibi mwa Tanzania .

Kati ya kipindi cha mwezi wa 12 mwaka jana hadi kufikia mwezi wa pili mwaka huu watoto 847 wameambukizwa surua kwenye wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga ameiambia BBC hadi sasa wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watoto 16480 na wanaendelea na zoezi hilo .

Pamoja na kutoa elimu wakiwataka wananchi wa eneo hilo kuachana na imani potofu kuwa vifo hivyo vimetokana na imani za kishirikina na badala yake wasikilize na kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya pamoja na kuwapelekea watoto kupata chanjo .

Ugonjwa wa surua huathiri watu wa rika zote japokuwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndio huathiriwa zaidi na dalili zake ni homa kali, udhaifu wa mwili pamoja na upele.

Miezi mitano iliyopita Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza mlipiko wa ugonjwa wa surua nchini Tanzania na kuanza kampeni ya utoaji chanjo ya surua na rubela kwa watoto walio chini ya miaka mitano nchi nzima.

Chanzo: Bbc