Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watajwa kula kiwango kidogo cha nyama

24939 PIC+NYAMA TanzaniaWeb

Thu, 1 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya Tanzania kushika nafasi ya pili Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na kuzalisha nyama kwa wingi, ulaji wa nyama kwa raia wake umeendelea kuwa chini ya kiwango kinachoelekezwa kiafya kwa binadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Chakula duniani (FAO) Mtanzania anakula wastani wa kilo 15 za nyama kwa mwaka wakati kiwango kinachotakiwa ni kilo 50.

Kufuatia hilo bodi ya nyama Tanzania imeweka mikakati ya kuhakikisha watanzania wanaelimika na kuanza kula kitoweo hicho kinachotajwa kuwa na virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini.

Kaimu Msajili wa bodi hiyo,  Imani Sichalise  amesema upungufu wa kilo 35 ni mkubwa hivyo ni muhimu kwa watanzania kuhakikisha wanakula nyama bora na salama kwa ajili ya afya.

Kuhusu madai kuwa nyama nyekundu ina madhara amesema hilo hutokea endapo itakuwa kwa kiwango kikubwa na itakuwa haijahifadhiwa katika mazingira salama.

“Nyama bora ni ile inayotokana na mifugo iliyotunzwa kwa kuzingatia viwango vya uzalishaji bora. Pia nyama inatakiwa iuzwe kwenye mabucha yaliyokidhi vigezo, usile nyama ya mezani au inayotembezwa mtaani”

Kwa mujibu wa ofisa wa nyama wa bodi hiyo Edgar Mamboi nyama iliyolala si salama.

Chanzo: mwananchi.co.tz