Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania takriban 400,000 wamepata Chanjo ya Covid-19

Gerson Msigwa 2?fit=1080%2C720&ssl=1 Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati zoezi la utowaji chanjo ya ugonjwa wa Corona nchini likiendelea kwa kasi nchini Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema, awali vituo vilikuwa 550 Nchi nzima na sasa tumefanikiwa kupanua wigo wa vituo na kufika zaidi ya 6,784 Nchi nzima.

Lengo likiwa ni kumfikia kila mtanzania aliye radhi kupata Chanjo ya Corona asipate shida kupata kituo cha kuchanjia katika eneo la karibu yake.

"Tunaweka chanjo kila sehemu zenye mzunguko wa watu wengi sokoni, vituo vya kupimia uzito wa magari, hata jana kwenye mechi ya watani wa jadi chanjo zilikuwepo ", amesema Gerson.

" Hata hivyo zoezi la Utoaji chanjo linakwenda vizuri na mpaka leo Watanzania takribani 400,000 wamechanjwa, kasi hii imeongezeka baada ya Wizara ya Afya, TAMISEMI na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuzindua Awamu ya Pili ya Uhamasisha na utoaji elimu" amesmea Gerson

Serikali inakamilisha utaratibua wa kuleta Chanjo nyingine Million 2 kutoka nchini China itwayo (SINOPHARM) mwanzoni mwa Mwezi ujao zitakuwa zimefika Tanzania.

"Watanzania msiopenda kuchoma sindano ni vyema mchukue nafasi hii kupata chanjo ya J$J amabayo unachoma mara moja kabla hazijakwisha kwakuwa Chanjo aina ya SINOPHARM unatikwa kuchoma mara mbili" , amesema Gerson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live