Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania 940,507 wapata chanjo ya Corona

Watanzaniapickl Watanzania 940,507 wapata chanjo ya Uviko-19

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

ais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Watanzania 940,507 tayari wamepata chanjo ya Uviko-19, sawa na asilimia 88.9 ya chanjo zilizopokelewa awali.

Hayo ameyasema leo Jumamosi Oktoba 16, 2021 wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya Yubile ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini (KCMC).

"Hadi kufikia Oktoba 15, 2021 jumla ya Watanzania 940, 507 wamechanja, sawa na asilimia 88.9 ya mzigo wa chanjo tulioupokea awali, niwahakikishie wananchi, Serikali inaendelea kuwezesha upatikanaji wa chanjo," amesema Rais Samia.

"Niwakumbushe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19, sina haja ya kusema mengi hapa Moshi, takwimu tulizonazo zinaonyesha jinsi Moshi ilivyoathirika na ugonjwa huu.

"Niwahimize wananchi kuchanja na kuchukua tahadhari zote kujiepusha na athari kubwa za ugonjwa huu, kwani kwa mujibu wa wataalamu hili ugonjwa bado lipo na hatujui lini litatoweka kabisa ulimwenguni," amesema.

Awali akiongoza ibada ya shukrani ya Yubile ya miaka 50, Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ugonjwa wa Uviko- 19 ambao umekuwa ni janga la dunia.

" Rais wetu na mama Yetu Samia Suluhu Hassan tunakushukuru na kukuunga mkono mia kwa mia katika kipindi hiki kwa namna unavyopambana na ugonjwa wa uviko 19 maana umekuwa mstari wa mbele," amesema Askofu Shoo.

"Nimehuzunika kusikia baadhi ya viongozi na hata wa dini kuhamasisha watu kutofuata taratibu za kujikinga na ugonjwa huu, Rais Samia Mungu amekuweka kipindi hiki kwa neema yake tunakushukuru na tunakuunga mkono," amesema Askofu Shoo.

Chanzo: mwananchidigital