Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania 207,391 wameshapata chanjo ya COVID-19

Makubi  Ed Katibu Mkuu Wizara ya afya, Profesa Abel Makubi

Mon, 16 Aug 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Serikali imesema mpaka kufikia jana jumla ya walengwa 207,391 wamepatiwa chanjo ya kukinga maambukizi ya corona.

Takwimu hizo zinaonyesha wanaume wamechanjwa kwa asilimia 58.3 sawa na 121,002 na 86,389 wakiwa ni wanawake sawa na asilimia 41.7.

Taarifa iliyotolewa Agosti 15, 2021 na Katibu Mkuu Wizara ya afya, Profesa Abel Makubi kuhusu maendeleo ya utoaji wa chanjo ya Covid-19 kwa wananchi imeeleza kuwa Serikali inaendelea kuratibu utoaji wa chanjo hiyo kupitia vituo vya kutolea huduma za afya vya umma na binafsi 550 vilivyoidhinishwa hapa nchini.

Amesema hadi kufikia Agosti 14 jumla ya dozi 1,008,400 za chanjo zilikuwa zimesambazwa katika mikoa yote 26.

“Tathimini ya utoaji chanjo tangu mikoa yote izindue, inaonesha mpaka kufikia jana jumla ya walengwa 207,391 wamepatiwa chanjo katika vituo vyote.

“Natoa maelekezo kwa watoa huduma wote, kutumia dakika chache kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kila mteja atakaye mhudumiwa kwa magonjwa mengine ili kumpa nafasi ya uelewa na baadae yeye kuchukua maamuzi sahihi juu ya chanjo,” amesema Profesa Makubi.

Profesa Makubi amesema pasiwepo na sababu yoyote ya wananchi waliofika vituoni kukosa au kukataliwa kupata huduma ya chanjo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz