Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wa familia moja walazwa kwa kula sumu

13736 Pic+sumu TanzaniaWeb

Fri, 24 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora.Watu watano wa família moja wamelazwa hospitali ya wilaya ya Urambo baada ya kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu.

Akizungumza leo Agosti 24 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kamgembya, kata ya Nsenda wilayani Urambo.

Amesema wanafamilia hao watano waliolazwa hospitali ya wilaya wanaendelea vizuri na hakuna yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz