WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema mashine za kupimia virusi vya corona zimepelekwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na jijini Arusha ili kuondoa adha kwa watalii wanaotembelea vivutio vya utalii.
Aliwambia waandishi wa habari kuwa, wadau wa utalii wanahitajika kushikamana ili kukuza sekta ya utalii wakati huu kutokana na janga la virusi vya corona.
Alisema jijini Dar es Salaam kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, itaendelea kusogeza huduma kwa watalii ili kuukabili ugonjwa wa Covid- 19.
Alizitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na watalii kupata huduma za vipimo vya corona katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti tofauti na awali ilivyokuwa ikipatikana Dar es Salaam pekee.
Alisema watalii wanaotembelea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti watakuwa wakipimwa corona na baada ya hapo watakwenda kutalii huku wakisubiri majibu ya vipimo vyao.
Awali, watalii walilazimika kukaa Dar es Salaam hadi majibu vya vipimo yatoke ndipo waande kutalii. Dk Ndumbaro alisema wizara hiyo imepeleka mashine mkoani Arusha kupimia virusi vy corona ili kuwawezesha watalii kupata huduma hiyo.
Alisema mashine hizo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mkoani Arusha ni jitihada za wizara hiyo kwa makubaliano na Wizara ya Afya ili kuwaondolea usumbufu watalii.
Dk Ndumbaro alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kutaka kuunda timu ya kuchunguza kwa namna gani serikali inaweza kukabiliana zaidi na ugonjwa wa Covid- 19.
Alitoa mwito kwa wadau kuendelea kuzingatia mwongozo wa mwaka jana Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kujikinga na virusi vya corona.
Dk Ndumbaro alisema Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutangaza vivutio vya utalii nchini na kwamba, hivi karibuni watalii 15 waliwasili wakitoka Israel.
Alisema Mei mwaka huu, Wizara inatarajia kupokea kundi lingine la watalii kutoka nchini humo. “Tunapambana usiku na mchana katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika katika nchi nyingi duniani ili tupate watalii wengi zaidi” alisema na kuongeza; “Ukiona sisi utalii umeshuka, basi kwa wenzetu huko hali ni mbaya sana kwa sababu watalii wengi ni wasafiri wa kutoka nchi za nje, nchi nyingi zimefunga mipaka yao, nchi nyingi zimefanya karantini,” alieleza.
Dk Ndumbaro alionya kuacha kukihusisha kila kifo na corona na kuposti kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikiharibu taswira ya n