Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalaamu 73 washiriki mafunzo kujilinda na mionzi

5830c999d0057649ac01f47c812b3d21 Watalaamu 73 washiriki mafunzo kujilinda na mionzi

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JUMLA ya wataalamu 73 wanaotoa huduma katika vyanzo vya mionzi kwa ajili ya uchunguzi na tiba kutoka hospitali mbalimbali hapa nchini wanashiriki katika mafunzo ya Kitaifa ya Usalama wa Mionzi yanayoendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) jijini Arusha.

Mafunzo hayo yaliyoanza jana, Jumatatu (Desemba 14, 2020) ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika mwaka jana 2019.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Mionzi wa TAEC, Dk Justine Ngaile amewataka washiriki hao kutumia uelewa watakaopata katika mafunzo hayo na kuhakikisha wanalinda afya za Watanzania ili wasipate madhara yatokanayo na mionzi.

Dk Ngaile amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea washiriki ufahamu juu ya matumizi salama ya mionzi na jinsi ya kujikinga na madhara ya mionzi.

Mafunzo pia yanalenga kuwasaidia washiriki kutambua viwango vya mionzi ambavyo ni salama kwa wafanyakazi katika maeneo ya kazi ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mionzi.

“Hii ni pamoja na kufuata sheria za usalama wa mionzi mahala pa kazi bila kusahau kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelekeza namna salama ya matumizi ya mionzi,” amesema

“Mtajifunza kwa kina masuala ya usalama wa mionzi katika maeneo ya kazi kwani usalama wa mionzi ni nyenzo muhimu katika kulinda wagonjwa, wafanyakazi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi. Hivyo basi, naamini mtajengewa uwezo mkubwa na watalaamu wa TAEC,” amesema Dk Ngaile.

Mkurugenzi huyo wa udhibiti amewahakikishia washiriki kwamba TAEC itaendelea kutoa mafunzo ya namna hii katika kuhakikisha inawalinda Watanzania dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza wakati vyanzo vya mionzi vinapotumika katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwandani, katika migodi, kwenye ujenzi, maeneo ya utafiti na katika vituo vyote vya afya vinavyotoa huduma kwa kutumia mionzi hapa nchini

Chanzo: habarileo.co.tz