Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Watakiwa kutoa elimu kuhusu bima ya afya’

4302585817a4f94ee6c92626724bb5b3 ‘Watakiwa kutoa elimu kuhusu bima ya afya’

Tue, 15 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt Ntuli Kapologwe amewataka waganga wakuu wa mikoa na halmashauri nchini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ilioboreshwa (CHF).

“Faida ya CHF iliyoboreshwa ni kuwa imeongeza wigo mpana wa upatikanaji wa huduma kwani ukiwa na hiyo bima popote pale ulipo nchini unaweza kupatiwa huduma za afya tofauti na awali katika eneo ulilojiandikisha,”amesema Dkt Kapologwe

Kapologwe amesema taratibu za kujiunga na bima hiyo ni kwamba mwananchi anakwenda kujiandikisha katika ofisi za mitaa, vijiji, vitongoji na mawakala walio katika maeneo yao ili kujiunga bila vikwazo.

Amesema utafiti ulifanyika kuweza kujua ni kiasi gani mwananchi anaweza kumudu ili aweze kuchangia ambapo asilimia 98 walisema wana uwezo wa kuchangia Sh 30,000 kwa mwaka mmoja isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao ada ni Sh 150,000 kwa kaya moja yenye idadi ya watu sita na Sh 40,000 kwa mtu mmoja.

Chanzo: habarileo.co.tz