Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuchangia damu Muhimbili

Profesa Janabi Watakiwa kuchangia damu Muhimbili

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuchangia damu.

Prof Janabi ameyasema hayo leo Julai 19, 2023 akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Mloganzila wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoratibiwa na klabu ya Yanga ikiwa ni utaratibu wao kuelekea kilele cha siku ya wananchi Julai 22 katika dimba la Benjamini Mkapa.

Janabi amesema kampeni hiyo Yanga ni moja ya tukio kubwa la hisani kwani uhitaji wa damu ni mkubwa.

“Hizi damu ndio zinatusaidia kufanya opereshni, wakina mama wanaojifungua, na wengine wenye uhitaji, ukitoa damu damu yako inarudi, ukiweka tabia ya kuchangia damu labda mara tatu au nne sio kwamba inaondoka inajizalisha upya.

“Ninawapongeza sana Yanga kwa tukio hili muhimu na niwaombe TFF wahamasishe na timu nyingine za ngazi zote kujitoa kwa jamii.” amesema Prof.Janabi”

Katika hatua nyingine Prof Janabi ametoa elimu juu ya baadhi ya wagonjwa kucheleweshewa huduma ya kupata damu.

“Watu wengi wanalaumu kwanini wagonjwa wao hawapatiwi huduma wakati huohuo ipo hivi damu unayotoa inakwenda kupimwa magonjwa mbalimbali, ni mchakato mrefu, tukishachukua damu tunaifanyia vipimo ili kuwa na damu salama ninaomba watu wafahamu hizo hatua” amesema Prof Janabi.

Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said amesema wameitenga siku ya jumatano ya Julai 19, 2023 kuwa siku muhimu ya kihistoria kwao kuokoa Maisha ya wenye uhitaji ili kuonesha dhana halisi ya kuwa mwananchi.

“Kinachofanywa na wanachama wa Yanga ni uungwana uliopitiliza, wapo watu wanaotoa damu lakini wanatoa kwa wagonjwa wanawaohusu tuu, lakini huu uungwana unaofanywa na wanachama wa yanga ambao hawajui damu wanayochangia anaipata nani, ni lazima jamii inayotuzunguka ipate mchango kutoka Yanga isiwe tuu kwamba sisi ndio tunapata kutoka kwao,” amesema Hersi.

Yanga wapo kwenye maandalizi ya kilele cha siku ya mwananchi itakayofanyika Julai 19, 2023 katika dimba la Benjamini mkapa ambapo watacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kazier Chiefs ya Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live