Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuchangia bima za afya kwa watoto

Bima Pc Data Watakiwa kuchangia bima za afya kwa watoto

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wananchi mkoani Rukwa, wameombwa kujitokeza na kuchangia upatikanaji wa bima za afya kwa watoto yatima, waliopo katika vituo vya malezi ili wawe na uhakika wa kupata matibabu.

Akizungumza leo Februari 15 baada ya kupokea msaada kutoka kwa wana kikundi cha kuweka na kukopa (Sacco’s) cha Twavwanwaje, mlezi mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Martin De Poles Katandala cha mjini Sumbawanga, Sista Agatha Kasanyi amesema, msada huo ni sehemu ya kuadhimisha miaka minane tangu kuanzishwa kwa Saccos hiyo.

Amesema bajeti ya uendeshaji wa kituo hicho ni zaidi ya Sh50 milioni kwa mwaka, huku fedha nyingi zikitumika kwenye matibabu ya watoto wanaolelewa kituoni hapo kwa kuwa wengi wao hawana bima za afya Kwa ajili ya matibabu.

"Tuna watoto wachache ndio wana uhakika wa kupata matibabu pindi wanapougua maradhi mbalimbali kwa sababu wana bima za afya, sasa tunaiomba jamii pamoja kutusaidia mahitaji mengine muhimu itusaidie pia kuhakikisha hawa watoto wanapata bima za afya kwa ajili ya matibabu yao," amesema Sista huyo.

Pia, ameeleza kusikitishwa kwake na kukithiri kwa visa vya kikatili dhidi ya watoto vinavyotokea mkoani humo kwa kuwa vinachangia sana ongezeko la watoto wa mitaani na yatima, akitaka vikomeshwe.

Awali, Mwenyekiti wa Sacco’’s ya Twavwanwaje, John Mahinya amesema wametembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali kwa kuwa wanatambua malezi ya watoto hao ni jukumu la jamii nzima na sio waanzilishi wa kituo pekee

Advertisement Amesema kwa jamii inapaswa kujenga utamaduni wa kuwatembelea watu wenye mahitaji na kuwatia moyo na kuwapa faraja ikiwa ni sehemu ya ibada na hata vitabu vya dini vinaeleza hivyo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz