Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuchagia damu kuokoa maisha ya majeruhi, wanawake

Blood Bags.webp Watakiwa kuchagia damu kuokoa maisha ya majeruhi, wanawake

Mon, 15 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WATANZANIA wametakiwa kuendelea kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya majeruhi na wanawake wanaojifungua ambao wana uhitaji mkubwa wa damu wakati wowote.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma Shirikishi za Tiba kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk. Lulu Sakafu, ametoa wito huo leo Juni 14 katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Mloganzila, jijini Dar es Salaam.

Amesema mahitaji ya damu ni makubwa kwa majeruhi wa ajali, wanawake wanaojifungua, wagonjwa saratani na figo ukilingamisha na makundi mengine hali inayosababisha uhitaji kuendelea kuongezeka kulingana na idadi ya wagonjwa.

“Mahitaji ya damu ni makubwa Muhimbili ndio maana tukaiomba wizara, damu salama na kukubaliana tuwe na kitengo cha kukusanya damu pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kujitoa zaidi. Idadi ya wagonjwa inavyoongezeka ndivyo uhataji unavyoongezeka," amesema Dk. Sakafu.

Dk. Sakafu pia amesema kuwa upungufu wa damu ni chupa 20 hadi 30 kwa siku katika hospitali ya Muhimbili na kwamba katika hospitali ya Mloganzila idadi ya wagonjwa wanaopokelewa ni waliopata ajali kwa sababu ipo jirani na barabara kuu ya Morogoro.

Kadhalika kwenye maadhimisho hayo, Dk. Sakafu amewakabidhi vyeti vya utambulisho pamoja na zawadi nyingine wachangiaji wa damu wa mara kwa mara ili kuongeza hamasa ya uchangiaji damu kwa hiari.

Naye Ofisa Mhamsishaji wa Damu kutoka hospitali ya Taifa Muhmbili-Mloganzila, John Daniel, amesema mahitaji ya damu yanaendelea kuongezeka kwa kuwa wagonjwa wenye magonjwa ya muda mrefu na wanaolazwa wapo kila siku.

“Mtu akiwa na damu pungufu labda ana damu tano, huyu ataongezewa damu hivyo benki ya damu lazima iwe damu muda wote kwa ajili ya watu kama hawa,” amesema Daniel.

Moja wa wachangia damu, Maxmillian Sekezia, ameiomba Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuwapatia huduma za bima ya afya bure kwa wachangiaji damu wa muda mrefu ili kutoa hamasa kwa watu wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live