Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaopata virusi vya Corona Tanzania kutibiwa mikoa hii

93631 Pic+corona Watakaopata virusi vya Corona Tanzania kutibiwa mikoa hii

Thu, 30 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri ya Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema mtu yeyote atakayepata virusi vya Corona nchini atatibiwa katika maeneo yaliyotengwa yaliyopo mkoani Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza.

Mlipuko wa virusi hivyo ulioanzia China hadi jana watu 106 wameripotiwa kufariki dunia huku zaidi ya 4000 wakiambukizwa.

Akizungumza mjini Dodoma leo Jumatano Januari 29, 2020 Ummy amesema. “maeneo hayo ni Mawenzi (Kilimanjaro), Buswelu ( Mwanza) na Kigamboni (Dar es Salaam). Wizara inaendelea kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huu endapo utaingia nchini. Tutahakikisha tunapata vifaa kinga, dawa na vifaa tiba vya kutosha.”

Amesema wanafanya uchunguzi kwa wasafiri wote kutoka Bara la Asia, kwenye mipaka  na wanaoingia nchini kupitia viwanja wa ndege vilivyopo Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Ummy amesema wanafanya uchunguzi katika bandari ya Dar es Salaam, wiki mbili zilizopita waliwachunguza watu 1520 walioingia nchini kutokea China kupitia bandari hiyo na waliotumia mipaka mbalimbali na viwanja vya ndege.

Ummy amesema Wizara inavyo vipima joto 140 ( vya mkono 125 na vya kupima watu wengi kwa Mpigo 15 ) vilivyofungwa kwenye mipaka.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz